Upendo wa kweri sio tu maneno mazuri, na wala sio tu upendo wa matendo au wa kuleta maua na chokleti.
Bali ni kuonyeshana heshima uaminifu na imani. Kuonyesha wepesi wa kuona huruma wakati mwanzako anapokuwa na msongo/matatizo. Kuwa msaidizi mwema na mwenye kusema ukweli. na kuweza kuonyesha masikitiko yako kwa mwenzio.
Sio kila wakati kujifanya mwenye nguvu (mvumilivu)/ mjuaji wa kilakitu, bali mkae/kaeni pamoja, mtatue issues pamoja, msaidiane pale mwenzako ameshindwa.
Usiwe wewe bali Kuweni ninyi kwa kila kitu mfanyacho. Muwe kila wakati mna furaha . Kama mmoja wenu ana uzuni basi uzunikeni pamoja.
Mshirikiane katika raha na shida, taabu na njaa kwenye maisha yenu.
No comments:
Post a Comment